Zoezi la kutoa huduma za macho bure kwa wakazi wa Halmashauri ya Mji Ifakara linakamilika leo Jumamosi tarehe 21 Septemba 2024.
Zoezi hilo lilianza tarehe 17 Septemba ,2024 ambapo litakamilika siku ya leo.Mpaka Sasa jumla ya wagonjwa 755 wamepatiwa huduma hiyo inayotolewa na Hospitali ya Halmashauri ya Mji Ifakara, iliyopo kata ya Kiberege.
Lengo la zoezi hilo ilikua ni kusaidia kuboresha afya ya macho kwa jamii na kutoa fursa kwa watu wengi kupata huduma hizi muhimu bila malipo.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa