CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) KUWEZESHA VIJANA KUONGEZA UZALISHAJI NA MNYORORO WA THAMANI WA MAZAO KATIKA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimetambulisha Rasmi Mradi wa TAGDev 2.0 AGRIFOSE -RIH, unaotekelezwa chini ya RUFORUM kwa ufadhili wa Mastercard Foundation kwa Vikundi 18 vya Vijana katika Halmashauri ya Mji Ifakara, Mkoani Morogoro.
Utambulisho huo umefanyika Leo Jumatatu Oktoba 6.2025 umehusisha Vikundi vya Vijana kutoka Kata nne za Kiberege, Katindiuka, Kisawasawa na Signal ambapo Mradi huo unalenga kuongeza uzalishaji na Mnyororo wa thamani wa mazao ya Mpunga na mbogamboga ukiwapa kipaumbele Vijana wakike wanaounda zaidi ya asilimia 70 ya Walengwa.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo , Mratibu wa Mradi kutoka SUA , Dkt. Hamisi Tindwa alisema Mradi huo utawajengea Vijana uwezo wa kuendesha biashara katika Sekta ya Kilimo badala ya kubaki katika uzalishaji pekee.
"Mradi huu utamwezesha Kijana sio tu kuzalisha , bali pia kuchakata mazao na kushiriki katika biashara. Baada ya miaka mitano ya utekelezaji wake, kuanzia Januari 2025 hadi Desemba 2029 tutapima mafanikio kwa idadi ya biashara mpya zitakazozaliwa kupitia Vijana hawa ". AlisemA Dkt. Tindwa
kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika warsha hiyo aliwapongeza Vijana waliochaguliwa kushiriki katika Mafunzo hayo, akiwataka kutumia maarifa watakayopata kuongeza ubunifu, matumizi ya teknolojia na masoko ya bidhaa zao.
"Nataraji kuona Vijana hawa wakibadilika na kutumia teknolojia za Kisasa katika uzalishaji na biashara ya mazao yao. Huu ni mwanzao wa mabadiliko makubwa katika uchumi wa Vijana wetu" . alisema Mhe. Kyobya
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bw. Said Majaliwa aliishukuru SUA kupitia Mradi wa RUFORUM kwa kuona umuhimu wa kuwawezesha Vijana katika Sekta ya Kilimo, akibainisha kuwa elimu hiyo italeta tija kubwa kwa jamii.
Mmoja wa Wasiriki wa Mafunzo hayo , Bi. Consolata Fabian kutoka Kikundi cha Promise cha Kisawasawa , alitoa shukrani kwa SUA kwa ujuo wa Mradi huo, akisema utawasaidia kupata maarifa mapya na kuongeza kipato kupitia shughuli za Kilimo Biashara.
Mradi wa TAGDev 2.0 AGRIFOSE -RIH ni sehemu ya Programu ya RUFORUM inayotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), Chuo cha Nelson Mandela (ARUSHA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaama (UDSM), na Jukwaa la Vyuo Vikuu Afrika (RUFORUM) kwa ufadhili wa Mastercard Foundation.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa