MIPANGO YA BAADAYE ( KUONGEZA UANDIKISHAJI UFIKIE 81%)
1.Kuingiza katika bajeti za Halmashauri fedha ya kuwalipia kaya ambazo hazina uwezo kama vile Watoto Walio Katika Mazingira Hatarishi, Walemavu na Wazee wasiojiweza.
2.Kuwashawishi waheshimiwa Madiwani na viongozi wa Serikali za Vijiji/ Mitaa kuonyesha mfano kwa kujiunga na CHF, hata kama wanazo kadi za NHIF, basi wawalipie ndugu na jamaa zao ambao bado hawajajiandikisha na CHF Iliyoboreshwa.
3.Maafisa Watendaji wa Kata walete kwa Mkurugenzi taarifa za CHF za kila mwezi ili kuwapima mwenendo wao wa utekelezaji.
4.Kuendelea kufanya uhamasishaji ili wananchi wajiunge na CHF, kwa kutumia Radio ya Halmashauri Kilombero na Pambazuko na vilevile kumtumia Afisa Habari wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara katika kuhamasisha.
5.Kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya, Halmashauri ya Mji wa Ifakara, itapita katika Asasi za Serikali na zisizo za Serikali zifuatazo KPL, ILLOVO, TANAPA, BENKI zote, MITIKI n.k ili kuwashawishi wasaidie kulipia kaya zijiunge na CHF, hasa zile zisizojiweza kiuchumi.
6.Katika mgao wa Fedha za Mfuko wa Afya wa Pamoja ( BUSKET FUND) ambazo zimeletwa katika robo ya tatu ( Jan-Machi 2017), Halmashauri ya Mji wa Ifakara imepata Tsh 80,000,000/= ili iweze kutekeleza shughuli zake ambazo zilipangwa katika mwaka wa fedha 2016/2017. Kwa kuona umuhimu wa kuwapatia wananchi huduma bora, imemuliwa kwamba fedha hizi zote zinaenda kununulia dawa, hivyo basi hizo shughuli zingine tofauti na dawa zitatekelezwa katika robo ya ijayo (ya 4).
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa