BENKI YA CRDB YAKABIDHI VITI 50 NA MEZA 50 SHULE YA SEKONDARI MAHUTANGA
Benki ya CRDB imekabidhi Viti 50 na Meza 50 Shule ya Sekondari Mahutanga iliyopo Kata ya Lumemo Halmashauri ya Mji Ifakara leo Oktoba 8,2025 Ikiwa ni Sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja na utaratibu wa Benki hiyo kurudisha kwa Jamii .
Akizungumza wakati wa Makabidhiano hayo Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kati Bi. Chabu Mishwaro alisema Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja zoezi hilo linafanyika katika Kanda 8 nchi nzima Ili kuhakikisha Mwanafunzi anapokua darasani anapokea kile anachofundishwa katika Hali ya Utulivu .
Mgeni katika Hafla hiyo alikua Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya ambapo aliwashukuru Benki ya CRDB kwa kuipatia Shule hiyo Viti na Meza hizo kwani imewasaidia kupunguza adha ya Viti 183 na Meza 183 Hadi Kufikia Viti 133 na Meza 133 .
Nae Afisa Elimu Sekondari Bw. Folkward Mchami alitoa shukrani kwa Benki hiyo na kuwasisitiza Wanafunzi hao Kuzingatia kutumia na kutunza vizuri Ili na wadogo zao waje kuvitumia.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa