KAMATI YA USALAMA YA WILAYA YA KILOMBERO (KU) YAMPONGEZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA BI. PILLY KITWANA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI
Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Kilombero ( KU) leo tarehe 3 Oktoba 2025 wamefanya Ziara ya Kukagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Mji Ifakara ikiwemo kukagua Maendeleo ya Mradi wa nyumba ya Mkurugenzi na Nyumba za Wakuu wa Idara.
Ziara hiyo iliongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Bw. Abraham Mwaikwila akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya. Bwana Mwaikwila alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Pilly Kitwana kwa kusimamia na kufuatilia vizuri Mradi wa nyumba hizo ambao mpaka sasa umefikia hatua ya Ukamilishaji na muda wowote zitaanza kutumika.
Aidha Kamati hiyo ilitembelea Jengo la Utawala la Halmashauri ya Mji Ifakara ambapo walielekeza Wasimamizi wa Mradi huo kufanyia kazi Maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na Kamati hiyo ili kukamilisha Mradi huo kwa Haraka na muda uliopangwa.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa