"ZINGATIENI SUALA LA LISHE ILI KUBORESHA UKUAJI NA AFYA ZA WATOTO" .Lucas Mwilwapwa.
Wakazi wa Kata ya Kibaoni wametakiwa kuzingatia suala la lishe kwa kutumia vyakula vya asili hasa mbogamboga na matunda kwenye milo yao.
Hayo yamesemwa na Afisa Lishe wa Kituo cha Afya Kibaoni Lucas Mwilwapwa mapema wiki hii wakati walipokua wakiadhimisha siku ya Lishe katika Kituo cha Afya Kibaoni .
Timu ya wataalamu wa Lishe katika kituo cha Afya kibaoni pamoja na Mtendaji wa Kijiji wametoa elimu juu ya namna bora ya kupangilia mlo wa Kila siku hasa Kwa watoto,wajawazito na mama wanao nyonyesha.
Aidha Afisa Lishe wa kituo cha Afya kibaoni Bw.Lucas Mwilwapwa amesema kuwa kufuatilia mpangilio mzuri wa ulaji wa makundi yote ya vyakula Kuna leta faida mbalimbali hasa upatikanaji wa madini na vitamini ambayo huboresha afya za watoto hasa kipindi hiki cha magonjwa mlipuko na homa za matumbo.
"Mlo kamili ni kinga dhidi ya magonjwa yote, maana hufanya mwili kuwa imara kwenye kupambana na magonjwa pia Vitamin A ni matone muhimu kwa watoto kila baada ya miezi sita hivyo wazazi msipuuze, haya matone ni msaidizi wa mbogamboga," alisema Mwilwapwa na kuongeza kuwa
" Msisahau vidonge vya minyoo kwa kila mtoto mwenye mwaka mmoja na kuendelea, minyoo imekuwa sumu na kurudisha nyuma ukuaji wao leteni watoto wapate chanjo kwa wakati." alisema Mwilwapwa.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa