MENEJIMENTI YA HALMASHAURI YA MJI IFAKARA YAFANYA ZIARA KUTEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO
Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Mji Ifakara imefanya Ziara ya kutembelea Miradi Mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Mji Ifakara. Ziara hiyo imefanyika siku ya Alhamisi tarehe 18 Septemba 2025 ambapo iliongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara akiambatana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Bw. Abraham Mwaikwila.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Miradi iliyoletewa Fedha na Serikali zaidi ya Milioni 892.3 kwa mwaka wa Fedha 2024 -2025 kupitia BOOST na GPE LANES kwaajili ya Ujenzi wa Miradi Mipya ya Elimu ya Awali na Msingi ndani ya Halmashauri ya Mji Ifakara ikiwemo Ujenzi wa Shule Mpya, Madarasa , vyoo , nyumba za Walimu na Ujenzi wa Kituo cha Walimu (TRC) Mkamba na pia walitembelea Umaliziaji wa Jengo la Maabara OPD na Kichomea Taka katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Ifakara iliyopo Kiberege wenye thamani ya Shilingi Milioni 65,000,000/= na pia walitembelea kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Utawala.
Akizungumza katika Ziara hiyo Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Bw. Abraham Mwaikwila alipongeza hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ukamilishaji wa Miradi hiyo na kusisitiza kuongezeka kwa kasi ya utekelezaji ili kuendana na muda uliopangwa ili miradi hiyo iweze kuwasaidia wananchi wa Ifakara hususani katika kupunguza adha ya umbali mrefu kwa wanafunzi kufuata masomo na pia kuongeza ukaribu wa upatikanaji wa Huduma za Afya kwa Wakati.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Pilly Kitwana aliwasisitiza wasimamizi wa Miradi hiyo kuhakikisha Vifaa vinapatikana muda wote katika maeneo yote ya miradi na pia kuhakikisha miongozo , taratibu na kanuni zinafuatwa . Aidha alisisitiza kuongezeka kwa kasi ya ukamilishaji wa Miradi hiyo kulingana na hali ya hewa hususani katika hiki kipindi ambacho Mvua zinatarajiwa kuanza wakati wowote.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa