Mwenge wa Uhuru umendelea kukimbizwa Mkoani Morogoro tangu ulipowasili Aprili 20, 2024 hadi leo Aprili 26, 2024 umekwisha pitia miradi ya maendeleo mbalimbali katika Halmashauri saba kati ya Halmashauri Tisa za Mkoa wa Morogoro.
Aprili 26, 2024 Mwenge wa Uhuru umekimbizwa katika Wilaya ya Kilombero Halmashauri ya Mji Ifakara Mji na Kupitia Miradi ya maendeleo Nane yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bil. 1,586,216774.50.
Mchanganuo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo: nguvu za wananchi shilingi 23,600,000.00, Halmashauri shilingi 85,568700.00, Serikali Kuu 637949954.50 na wahisani au wadau wengine wa maendeleo wamechangia kiasi cha shilingi 839,098120.00
Moja ya miradiya maendeleo iliyotembelewa ni Pamoja na uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha Mhelule kilichopo Tarafa ya Mang’ula wilayani kilombero Mkoani Morogoro wenye gharama ya shilingi 542,989,954.5 baada ya kupata fedha kutoka mfuko wa Maji wa Taifa – NWF na utanufaisha wakazi wapatao 2,838
Akiwa katika eneo hili Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa alisitiza na kuwataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa huo kuandaa program maalum ya kuwawezesha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU) ngazi ya Wilaya ili waweze kuelewa vema mfumo wa NeST unavyofanya jambo litakalowarahisishia wajumbe hao kufuatilia mfumo huo kufanya kazi inavyotakiwa na hivyo kutoa matokeo Chanya na yanayotarajiwa na Serikali.
Katika hatua nyingine Mwenge huo wa Uhuru uliona shughuli za utunzaji mazingira zinazofanyika katika kando yam to Lumemo unaopita katikakati ya Mji wa Ifakara ambapo kulikuwa na kampeni ya takribani wiki moja na kufanikiwa kupanda miti 2000. Mwenge wa Uhuru nao ulifanikiwa kufika katika eneo hilo na kushirikiana na wananchi wa Mji wa Ifakara kupanda miti zaidi ya 1000 hivyo kufanya jumla ya miti iliyopandwa kufikia miti 3000.
Ujumbe wa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa wananchi sio kupanda miti tu, bali kupanda miti 1,500,000 kila mwaka kama maagizo ya Serikali ambavyo yalishatolewa lakini zaidi ni kutunza miti hiyo ikue na kuleta mafanikio tarajiwa ikiwa ni Pamoja na kupunguza chanagamoto mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni Pamoja na mafuriko ambayo yamekithiri pahala pengi duniani.
Mradi mwingine uliotembelewa ni Pamoja na Uzinduzi wa Ukumbi wa Mikutano kutoka Sekta binafsi ambapo amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira mazuri ya wawekezaji binafsi wa ndani nan
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa