Wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa wa Halmashauri ya Mji Ifakara wametakiwa kuhakikisha wanasikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi katika maeneo yao.
Hayo yamesemwa Januari 7 ,2024 na Afisa Tawala wa Wilaya ya Kilombero Phabius Byamungu alipokua akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya aliyekuwa Mgeni Rasmi wakati wa kufungua Mafunzo Elekezi kwa Wenyeviti wa Mitaa, Vitongoji na Vijiji katika Ukumbi wa Mlimba uliopo Halmashauri ya Mji Ifakara.
Aidha aliwataka Wenyeviti hao kuhakikisha wanasimamia suala la Ulinzi na usalama katika maeneo yao, kupambana na Rushwa, kupinga ukatili wa kijinsia, kusimamia Mazingira, kushiriki katika miradi ya Maendeleo na kuibua vyanzo vya mapato.
" Twende tukatende haki tukawasikilize Wananchi wetu, tukasimamie majukumu yetu,tunatarajia ninyi ndio muwe mfano na walimu mara baada ya Mafunzo haya". Alieleza Bw .Byamungu
Mmoja wa Wenyeviti hao Bw. Geoffrey Mtapika ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Njokamoni Kata ya Mang' ula aliishukuru Halmashauri ya Mji Ifakara kwa kuwapatia Mafunzo hayo kwani yatakua muongozo katika majukumu yao na kuahidi kuboresha maeneo yote yaliyokua na mapungufu .
"Ninashukuru kwa Mafunzo haya kwani yananipa mwanga katika Shughuli zangu za kiutendaji".Alisema Bw. Geofrey.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bw. Rashid Semngoya alisema Mafunzo hayo yameandaliwa kwa Viongozi hao Ili waweze kutambua majukumu yao na kufanya Kazi kwa ufanisi. Aidha Mafunzo hayo yalitolewa na wawezeshaji kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI) - Hombolo .
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa