Watendaji wa Kata 19 za Halmashauri ya Mji Ifakara wamekabidhiwa Pikipiki ikiwa ni njia ya kutatua changamoto ya usafiri iliyokua ikiwakabili watendaji hao hasa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Hafla hiyo imefanyika Jumamosi tarehe 16 Novemba 2024 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mlimba uliopo Halmashauri ya Mji Ifakara.
Pikipiki hizo zilinunuliwa mara baada ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi . Zahara Michuzi kukataa kununuliwa gari kutoka kwenye Fedha za mapato ya ndani kiasi cha Shilingi Milioni 186,000,0000 zilizokua zimetengwa kwaajili ya Ununuzi wa Gari la Mkurugenzi, Hivyo badala yake akaomba fedha hizo zielekezwe kwenye matumizi ya ununuzi wa Pikipiki za watendaji wa Kata 19 za Halmashauri ya Mji Ifakara, na kiasi kinachobakia kielezwe kwenye shughuli nyingine za miradi mbali mbali ya Maendeleo.
Hivyo kupitia Vikao mbalimbali vya kisheria vya Halmashauri, CMT na Madiwani wa Halmashauri ya Mji Ifakara kwa pamoja waliridhia ombi hilo la ununuzi wa Pikipiki 19 zenye thamani ya Shilingi Milioni 67,450,000 kwa ajili ya watendaji wa kata wote 19.
"Niliona Watendaji wa Kata wakipata shida ya usafiri katika kufikia maeneo mbalimbali katika Kata zao , na wakati mwingine kuchelewesha kuhudumia Wananchi kwa wakati na hata kushindwa kufikia vyanzo vyao vya mapato kwa ukamilifu, hivyo naamini kwa usafiri huu utawasaidia kusimamia kazi zao na Kutatua kero mbalimbali za wananchi". Alisema Bi. Zahara
Mtendaji wa Kata ya Mwaya Bw. Acley Mhenga alimshukuru Mkurugenzi huyo kwa kuwatatulia changamoto hizo na kuwasihi watendaji wenzake kuzitunza na kuzitumia vizuri Pikipiki hizo ili ziwe chachu ya kufanya Kazi kwa weledi na ufanisi zaidi.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikua Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Danstan Kyobya ambaye alimpongeza sana Mkurugenzi kwa uthubutu huo wa kuwajali watendaji wenzake wa kada ya chini kwa kuwaondolea adha ya muda mrefu ya kukosa usafiri, na kuwasihi kwenda kuzitumia Pikipiki hizo kwa Kazi za Serikali kwa kutatua changamoto na kero za Wananchi.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa