Mafunzo haya yalifanyika siku ya jumatatu tarehe 2,Disemba 2024 katika Tarafa ya Ifakara yakiwa na lengo la kuwawezesha wakulima kuboresha uzalishaji wa mazao ya mbogamboga na matunda kupitia mbinu za kisasa na endelevu.
Mafunzo hayo yaliendeshwa na Wataalamu kutoka Divisheni ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi, ambapo mada mbalimbali zilifundishwa ikiwemo Mbinu Bora za Kilimo (Good Agricultural Practices - GAPs),Uandaaji bora wa mashamba,Upandaji wa mbegu bora na matumizi sahihi ya mbolea,Usimamizi mzuri wa maji na udongo.
Sambamba na hilo pia walifundishwa Kilimo Huishi (Regenerative Agriculture) na Kilimo Endelevu (Sustainable Agriculture),Njia za kuboresha afya ya udongo na mazingira,Kupunguza utegemezi wa kemikali katika uzalishaji wa mazao na Kuongeza tija kwa kutumia rasilimali zilizopo,
Vilevile Matumizi Sahihi na Salama ya Viuatilifu Kwa Kuchagua viuatilifu vinavyokubalika kwa afya na mazingira pia mbinu za kutumia viuatilifu kwa usahihi ili kuzuia athari kwa mimea na afya ya binadamu pamoja na hifadhi na utupaji salama wa mabaki ya viuatilifu.
Mafunzo haya yamepokelewa kwa furaha na washiriki, wakitambua kuwa ni hatua muhimu katika kuboresha uzalishaji na uhakika wa chakula katika maeneo yao.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa