Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya leo tarehe 26 Novemba 2024 , ameongoza matembezi ya kuhamasisha Wananchi wa Kilombero kushiriki Uchaguzi kesho tarehe 27 Novemba 2024.
Matembezi hayo yaliandaliwa na Hospitali ya Mtakatifu Fransisko iliyopo Halmashauri ya Mji Ifakara .
" Hongereni sana St. Francis kwa jambo hili , niwaombe kila mwenye miaka 18 na amejiandikisha kwenye Daftari la Mkazi anawajibu wa kupiga kura hapo kesho". Alisema Mhe. Kyobya
Vilevile, matembezi hayo yalihudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mhe. Abubakari Asenga ambaye aliwataka Wananchi wa Kilombero kupiga kura hapo kesho kwani hutokea kila baada ya miaka mitano hivyo ni muhimu kufanya maamuzi na kuchagua viongozi watakao leta Maendeleo .
Aidha, katika tukio hilo Mkurugenzi wa Hospital ya St.Francis, Bw.Solanus Fussy alimkabidhi Mkuu wa Wilaya magari matano yatakayo beba wazee na watu wasiojiweza kuwapeleka Vituoni kupiga kura.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa