Ikiwa ni muendelezo wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria katika maeneo mbalimbali nchini katika Halmashauri ya Mji Ifakara wananchi wamepata fursa ya kuelimishwa kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria kupitia kampeni ya msaada wa kisheria inayojulikana kama Kampeni ya Mama Samia ya Msaada wa Kisheria.
Kampeni hii imelenga kuwasaidia wananchi kupata uelewa wa haki zao za kisheria, wajibu wao, na namna ya kushughulikia changamoto zinazohusiana na masuala ya sheria katika maisha yao ya kila siku.
Kupitia kampeni hii wananchi hao wamenufaika na elimu ya kukabiliana na changamoto za Mirathi,Ndoa, Haki za binadamu,matunzo Kwa watoto pamoja na Ukatili wa Kijinsia.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa