Wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Halmashauri za Ifakara,Mlimba,Ulanga na Malinyi wamehudhuria mafunzo ya mfumo wa Upimaji Utendaji kazi wa Taasisi - PIPMIS na yale ya Mfumo wa Upimaji Utendaji kazi kwa Watumishi wa Umma -PEPMIS
Mafunzo hayo yameanza leo Disemba 11,2025 hadi Disemba 16 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Ifakara yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, yakiwahusisha pia Wakurugenzi wa Halmashauri hizo.
Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe.Dunstan Kyobya,amewataka Watumishi hao kuzingatia mafunzo yanayotolewa kwani yataongeza umakini katika vituo vyao vya kazi na kutoa taarifa ya uwajibikaji wa kila siku. “Nawasihi watumishi mnaopata mafunzo haya ambayo yanafanyika nchi nzima hakikisheni mnatoa ushirikiano katika kuhakikisha tunafikia kusudio la serikali kufikia malengo yaliyowekwa.” Amesisitiza Kyobya.
Kwa Upande wake Afisa kutoka Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi na Umma Utawala bora ametoa maelekezo ya kuhakikisha usimamizi wa utendaji kazi katika Utumishi wa Umma unazingatiwa kwa kufuata vigezo wakati wote na upimaji wa utendaji kazi kwa watumishi wa serikali uzingatiwe.
Mifumo hii ya kielektroniki ya Usimamizi wa Utendaji kazi( PEPMIS na PIPMIS) pamoja na mfumo wa Tathmini ya rasilimali watu ili kujiridhisha kama majukumu yanatekelezwa ipasavyo imeanza tangu Septemba 2023 ambapo itasaidia kubaini hali ya mahitaji ya rasilimali watu,kufanya tathmini ya uhitaji wa Maafisa, wasaidizi na watumishi wanaohitajika ili kupata mahitaji sahihi ya watumishi wanaohitajika kwani mfumo utachakata wenyewe idadi ya mahitaji ya watumishi wanaohitajika.
Mbali na hayo Mifumo itasaidia maombi ya uhamisho kufanyika kwa urahisi, usimamizi wa Utendaji kazi,utoaji wa taarifa za uwajibikaji,upangaji wa malengo na shuhuli za idara husika pamoja na uombaji wa mikopo bila kupoteza muda na gharama zisizo za lazima.
Matukio Katika Picha:
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa