Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya amesema uwepo wa Kampuni ya Sukari Kilombero uwe chachu ya kuwanufaisha wakulima wa Miwa katika Wilaya hiyo .
Hayo ameyasema leo Alhamisi Februari 6, 2025 wakati alipokuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Wadau wa ndani wa Kampuni ya Sukari Kilombero akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima .Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Kampuni hiyo Kata ya Kidatu - Ifakara.
"Zone zifanyike vizuri ,teknolojia ya Uzalishaji iongezeke ili wakulima wazalishe kwa tija". Alieleza Mhe. Kyobya
Aidha Mkutano huo ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo( MB) ambapo aliwataka Viongozi katika Maeneo hayo kuwa daraja la kuwaunganisha Wananchi na Kampuni hiyo ya Sukari kwa kuendelea kudumisha amani , utulivu na mahusiano mazuri baina yao.
" Bonde hili linategemea muwa kama chanzo cha Uchumi, Viongozi mnakazi ya kusimamia amani na utulivu, kwenye utulivu na amani lazima kuwe na uzalishaji wenye tija". Alisisitiza Mhe. Londo
Aidha DC Kyobya alisisitiza kila AMCOS ihakikishe inapanda Miche ya Matunda 5000 na kuahidi kutoa miche bure kwa AMCOS hizo .Vilevile alieleza juu ya umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji ili kuondoa migogoro katika vyanzo hivyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Sukari Kilombero Bw. Derrick Stanley alieleza lengo la Mkutano huo ni kuboresha mahusiano baina ya Kampuni na Wadau wake na kuhakikisha mahusiano hayo yanaimarika zaidi.
" Niwapongeze wadau wetu kuhakikisha Kiwanda kinapata muwa kila siku, lengo kubwa ni kuhakikisha Kiwanda hiki kinapata muwa na Sukari ya uhakika". Alisema Bw. Derrick
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa