Viongozi wa vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) Halmashauri ya Mji Ifakara watakiwa kuhamasisha wakulima kujikita katika kilimo cha mazao ya kimkakati.
Akizungumza katika kikao kazi kilichofanyika mapema wiki hii Afisa ushirika Halmashauri ya Mji Ifakara Ndugu. Issa Kiluwa amewasisitiza viongozi wa vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kusaidia katika ukusanyaji wa zao la mbaazi ili wakulima waweze kuuza kwa bei nzuri kupitia mfumo wa stakabadhi mazao ghalani.
"Siku ya leo tumekutana na vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) Kwa lengo la kujadili au kutathimini msimu wa zao la Ufuta pia kujipanga na msimu unaokuja wa zao la Mbaazi kwani msimu huu Ifakara AMCOS tumeuza Tani 247.84",alisema Kiluwa.
Mmoja wa viongozi hao ndugu Edwin Daudi amewataka Ma Afisa kilimo kutoa Elimu ya kutosha Kwa wakulima ili waweze kulima kilimo chenye tija Kwa kuzitambua mbegu na mazao bora yatakayo wapatia kipato.
"Wakulima wanatamani kulima mazao ya kifedha yanayoweza kuwainua haraka pia ma bwana shamba inabidi wawe karibu na wakulima ili watambue mmea ni nini na unahitaji nini pia watu wengi bado wanalima kilimo cha zamani inabidi tubadilike."alisema Daudi
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa