"MKAISHI NA KUTII KIAPO MLICHOAPA" Mhe. Wakili Dunstan Kyobya
Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba wametakiwa kuishi kiapo walichoapa kwa kuzingatia utii, uaminifu, nidhamu, haki, na weledi wakati wa kutenda majukumu yao.
Hayo yamesemwa leo tarehe 15 Novemba 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Danstan Kyobya wakati alipokua akifunga Mafunzo kwa wahitimu hao wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba Kundi la 47 A , Kata ya Kibaoni Halmashauri ya Mji Ifakara.
" Msimuonee mtu mkatekeleze majukumu yenu kwa kutenda haki na kuzisimamia" . Alisema Mhe. Kyobya
Awali wakati akisoma taarifa kwa Mgeni Rasmi ,Mshauri Mkuu wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba Wilaya ya Kilombero Luteni Kanali Munisi alitaja miongoni mwa mambo waliyojifunza wahitimu hao ni ukakamavu, ujasiri , nidhamu, uaminifu ,utii, mapambano dhidi ya Rushwa , huduma ya kwanza n.k.
Mafunzo hayo yalifanyika kwa muda wa wiki 18 , jumla ya wahitimu 125 wamehitimu Mafunzo hayo wakiwemo wanaume 106 na Wanawake 19.
Mahafali hayo yalihudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Zahara Michuzi.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa