WADAU WA KILIMO ,MIFUGO NA UVUVI WATAKIWA KUWASAIDIA WANANCHI KUPATA MBEGU BORA
Rai hiyo Imetolewa Leo tarehe 26 Septemba 2025 na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Bw. Abraham Mwaikwila ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya kufungua Kikao cha Wadau cha Maandalizi ya Msimu wa Kilimo 2025/2026 katika Ukumbi wa Mikutano iliyopo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero ambapo alieleza kuhusu umuhimu wa kuwahusisha Wananchi katika Sekta ya Kilimo, Mifungo na Uvuvi Ili kuwakomboa Kiuchumi.
"Msifanye Kilimo cha Mazoea tufanye Kilimo cha kuwasaidia Wananchi kwa kuwapa Elimu ya mbinu mbalimbali za Kilimo , Mifugo na Uvuvi Ili Wainuke Kiuchumi". Alisema Bw. Mwaikwila
Awali Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bw. Said Majaliwa aliwaeleza wadau hao kushirikiana kujadili kwa kina Maandalizi ya Uzinduzi wa Msimu wa Kilimo 2025/2026 na Mpango Mkakati wa Sekta hiyo Yenye mchango mkubwa katika Mapato ya Halmashauri!
Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bw. Yuda Mgeni aliwasilisha Mpango Mkakati wa Uendelezaji Sekta hiyo ya Kilimo ,Mifugo na Uvuvi .
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa