WADAU MBALIMBALI WAHIMIZWA KUWEKEZA KATIKA UJENZI WA VIWANDA VYA KUCHAKATA TAKA ( RECYCLING) ILI KUZIONGEZEA THAMANI
Wadau mbalimbali wamehimizwa kuwekeza katika ujenzi wa Viwanda vya Kuchakata taka ( Recycling) ili kuongeza thamani ya Taka na Kupunguza Uchafuzi wa Mazingira.
Hayo yamesemwa leo Jumamosi tarehe 20 Septemba 2025 na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara, Bi. Pilly Kitwana wakati wa maadhimisho ya Siku ya Usafishaji Duniani yaliyofanyika sehemu mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Mji Ifakara ikiwemo stendi kuu ya mabasi,
Aidha wananchi kutoka sehemu mbalimbali walishiriki katika kufanya usafi maeneo mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, wadau wa mazingira, wajasiriamali, wakuu wa idara na vitengo, watumishi wa Halmashauri, viongozi wa kata na vijiji pamoja na watu maarufu.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni: “Tunza Mazingira kwa Kuzipa Taka Thamani.”
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Bi. Pilly Kitwana Amesisitiza kuwa Halmashauri ya Mji Ifakara iko tayari kutoa mazingira wezeshi kwa wawekezaji katika sekta hiyo.
“Nitoe wito kwa wadau kuendelea kuwekeza na kutafuta fursa katika uchakataji wa taka kwa kuziongezea thamani, hatua itakayosaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira. Kama Halmashauri yetu pendwa, tupo tayari kutoa mazingira wezeshi kuhakikisha utekelezaji wa kaulimbiu hii unafikiwa hapa Ifakara,” alisema Bi. Pilly.
Aidha, Mkurugenzi amewapongeza watumishi na wajasiriamali wa Soko la Kibaoni na maeneo mengine katika Kata kwa kushiriki kikamilifu katika zoezi la usafi wa mazingira kama sehemu ya maadhimisho hayo.
“Naendelea kusisitiza kuwa suala la usafi ni jukumu la kila mmoja wetu, kuanzia majumbani hadi maofisini. Nawapongeza sana kwa kujitokeza na kushiriki katika usafi wa soko letu la Kibaoni. Kama Halmashauri ya Mji Ifakara, tunaendelea kutekeleza kwa vitendo tumeshanunua gari jipya la taka ambalo linatarajiwa kuwasili hivi karibuni, hatua itakayosaidia kuboresha zaidi hali ya usafi katika mji wetu,” alisisitiza Bi. Pilly Kitwana.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa