Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara Mhe. Kassim Faya Nakapala amesema Ujenzi wa Soko la Kiberege katika Kata ya Kiberege Halmashauri ya Mji Ifakara unatarajiwa kukamilika hivi Karibuni kutokana na mradi huo kuendelea kutengewa bajeti ili kukamilisha ujenzi wake kwa Mwaka Mpya wa Fedha 2025/2026.
Hayo ameyasema Jumamosi tarehe 11 Januari 2025 wakati akijibu swali lililoulizwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Kilombero Ndugu, Mohammed Msuya kuhusu maendeleo ya Mradi huo wakati wa Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kilombero kupitia Utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Akijibu swali hilo Mhe. Nakapala alisema mpka sasa Mradi huo wa Soko la Kiberege tayari umetengewa pesa ya kukamilisha ujenzi wake katika bajeti ya mwaka 2025/ 2026 ambapo pesa hizo ni za Mapato ya Ndani ya Halmashauri na Mpaka kukamilika kwake Mradi utagharimu kiasi cha Shilingi Milioni 34,000,000.
" Ili miradi ikamilike Halmashauri inatakiwa kuongeza kasi ya Ukusanyaji wa Mapato kwani Mradi huo ni miongoni mwa miradi inayotegemea mapato ya ndani ili iweze kukamika ". Alisema Mhe. Nakapala
Sambamba na hilo , Mhe. Nakapala alieleza kuwa mpaka sasa Halmashauri imekusanya kiasi cha Shilingi 2, 874,097,273 sawa na asilimia 44 ya Makusanyo ya Fedha za Mapato yote ya ndani ambayo lengo lake la Makusanyo kwa bajeti ya mwaka wa Fedha 2024 /2025 ni Sh. 6, 587,395,510.
Aidha Muheshimiwa Nakapala alieleza baadhi ya Changamoto zinazokabili Halmashauri katika ukusanyaji wa Mapato na kueleza kuwa tayari Halmashauri imeshaweka mikakati ya kuongeza wigo wa Ukusanyaji wa Mapato na kuahidi kufikia lengo la asilimia 100 ya Ukusanyaji wa Mapato ifikapo mwisho wa mwaka wa Fedha 2024/2025.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa