Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilayani Kilombero tarehe 20 Septemba,2024 imekabidhi kazi ya ujenzi wa daraja la Mkasu kwa mkandarasi Dolphin Engineering (T) Limited aliyeshinda zabuni.
Ujenzi huu unatarajiwa kuboresha mawasiliano kati ya vijiji vya karibu na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na huduma.
Makabidhiano hayo yalifanyika mbele ya Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mhe.Abubakar Asenga Alipo kuwa katika Ziara yake katika Kijiji cha Mkasu kata ya Kiberege ambapo wakati wa hafla ya makabidhiano hayo meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) wilayani kilombero Mhandisi.Sadiki Karume alisisitiza umuhimu wa mradi huu katika kuendeleza uchumi wa eneo hilo.
Mkandarasi aliahidi kukamilisha kazi kwa wakati na kwa viwango vinavyokubalika, huku akisisitiza kuwa watazingatia ubora na usalama katika kila hatua ya ujenzi.
Aidha wanakijiji walifurahia hatua hiyo uku wakitarajia manufaa makubwa yatakayopatikana mara baada ya daraja hilo kukamilika.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa