Wadau wa kilimo,mifugo na uvuvi wamejitokeza kata ya Mwaya (uwanja wa Mashada) katika maadhimisho ya ufunguzi wa msimu wa kilimo 2023-2024 ambapo wadau hao wametakiwa kutumia njia za kisasa katika kutekeleza shughuli zao ili msimu huu uweze kuwa na mafanikio.
Aidha wadau wa kilimo wanakabiliana na changamoto za mlipuko wa vijidudu visumbufu vya mazao pamoja na uharibifu wa mazao unaotokana na mifugo pia wakulima wasio sajiliwa kukosa mbolea wanapokwenda kwa mawakala walio sajiliwa.
pamoja na changamoto zinazo wakabili wakulima Halmashauri ya mji Ifakara kupitia divisheni ya Kilimo ,mifugo na uvuvi inaendelea kutoa elimu kuhusu kanuni za kilimo bora ili kuongeza tija na uzalishaji.
Sambamba na hilo wataalamu wa kilimo kwa ngazi ya Halmashauri kuhakikisha viwatilifu vinavyouzwa vina ubora pia kuwezesha wakulima kulima kilimo cha kimkakati hasa zao la korosho.
Aidha Wakili Innocent Magesa Afisa tawala wilaya ya Kilombero ambae amemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Dunstan Kyobya amewataka wakulima kujitahidi kutumia elimu na maelekezo ya wataalam wanayowapatia.
"Kwakua tunatumia viwatilifu na mbolea na ili tupate tija ni lazima tufuate maelekezo na ushauri wa kitaalamu," amesema Magesa.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa