Wananchi wa Jimbo la Kilombero wametakiwa kushiriki katika Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotarajiwa kuanza kuanzia Tarehe 1Machi, 2025 hadi tarehe 7 Machi 2025 katika Kata zote 19 za Jimbo la Kilombero.
Akizungumza mara baada ya kikao na Makatibu wa Vyama vya Siasa wa Wilaya ya Kilombero kilichofanyika leo Februari 24, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Halmashauri ya Mji Ifakara,Afisa Muandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Jimbo la Kilombero Bw. Rashidi Semngoya ametoa Rai kwa kila mwananchi wa Jimbo la Kilombero mwenye sifa za kushiriki zoezi hilo kutumia haki hiyo ya Msingi kujiandikisha na kuboresha taarifa kwenye Daftari la wapiga Kura.
" Kila Mwananchi wa Jimbo la Kilombero mwenye sifa ajitokeze kuanzia tarehe 1 hadi 7 Machi kushiriki zoezi hili Ili aweze kumchagua kiongozi anayemtaka katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu". Alieleza Bw. Semngoya
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa