Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Ndg.Lena Nkaya ameeleza mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika Mkutano wa Vyombo vya Habari uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkoa wa Morogoro leo Novemba 2,2023.
Akibainisha hayo Ndg.Lena amesema kuwa katika sekta za Afya, Elimu, Maji na Miundombinu, changamoto mbalimbali za Wananchi zilizo watatiza kwa muda mrefu zimeweza kutatuliwa.
Hata hivyo katika sekta ya Afya Serikali imewezesha ujenzi wa vituo viwili vya Afya, Zahanati saba na vifaa tiba na kupelekea upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa ufanisi.
Sambamba na hayo katika sekta ya Elimu Sekondari imeboreshwa kwa kujengewa maabara 16,nyumba sita za watumishi ,shule mpya nane pamoja na mabweni kwa shule ya wasichana .
Kwa upande wa Elimu msingi Serikali imewezesha ujenzi wa shule tatu mpya,matundu ya vyoo 226 na madarasa 256 kwa shule zilizokuwa na uhaba wa madarasa na kuondoa tatizo la msongamano mkubwa wa wanafunzi darasani.
Si hayo tu lakini pia mafanikio kwa sekta za Kilimo na mifugo,Maji na miundombinu yameelezwa ikiwemo ujenzi wa Majosho, Maboresho ya minada na kuwepo kwa Mzani wa kupimia mifugo kabla ya uuzwaji.
Mkutano huo umehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Wakuu wa Wilaya za Morogoro,Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro ukiwa na lengo la utekelezaji wa Kampeni ya kutangaza mafanikio ya Serikali kwa miaka mitatu iliyozinduliwa Novemba 1,2023 Jijini Dodoma.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa