Kufuatia kukithiri Kwa wimbi la utapeli na wizi wa mitandaoni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa mafunzo Kwa Madiwani,Viongozi wa Serikali za Mitaa,vijiji na Kata wa Halmashauri ya Mji Ifakara.
Semina hiyo ya Mapambano dhidi ya utapeli wa Mitandaoni iliandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mhe.Abubakary Asenga ambapo alisema kuwa kumekuwa na wimbi la utapeli wa Mitandaoni katika jamii zetu.
Aidha Mhe. Asenga amesema kuwa lengo la kuwaita viongozi wa Serikali za Mitaa, vijiji na Madiwani ni kujadili Kwa pamoja ni namna gani wanaweza kutatua changamoto hii lakini pia kufikisha ujumbe Kwa jamii zinazowazungukuka kuhusu suala la utapeli na wizi wa Mitandaoni.
Hata hivyo Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kilombero SP Daudi Nkuba ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuwadhibiti watoa huduma za kusajili line ambao wamekuwa chanzo kikubwa cha uwepo wa vijana wanaojikita katika kutafuta pesa kwa njia zisizofaa maarufu kama (Halohalo).
"hakuna uhalifu unaotuumiza Ifakara na Kilombero kama halohalo,sasa hivi kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wakijishughulisha na vitendo hivi vya uhalifu wa Mitandaoni na Kuna baadhi ya Wazazi au walezi ambao wanachochea watoto wao kufanya wizi huu," Alisema SP Nkuba.
Meneja wa kitengo cha masuala ya wateja na watumiaji wa huduma za Mawasiliano (TCRA) mhandisi Kadaya Baluhye Amesema kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania haijihusishi na Michezo yeyote ya bahati na sibu pia Kuna umuhimu wa Wazazi kufuatilia tabia na mienendo ya watoto wao ili kudhibiti kujikita katika makundi yasiyofaa.
"Ulinzi na Usalama ni jukumu letu sote, Mbunge anataka kuwa na jamii inayofaa ndio maana tumekuja kutoa elimu hii Kwa wakazi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Kila mmoja ana wajibu wa kulinda na kutumia Mawasiliano Kwa ufasaha
Naye Mkuu wa Wilaya Kilombero Mhe.Wakili Dunstan Kyobya amesema kuwa anahitaji Ifakara ibadilike Kwa Kila Kijiji na Mtaa kuwe na daftari la wakazi ili kuweza kutambuana,Sambamba na hilo amesisitiza viongozi waliohudhuria semina hiyo kwenda kuwa mabalozi na kutoa Elimu Kwa jamii dhidi ya utapeli wa Mitandaoni.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa