Wadau mbalimbali na Wananchi kwa ujumla wametakiwa kujitokeza kushiriki kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya wakati akizindua zoezi la upandaji miti la Shirika la SOLIDARMED katika eneo lililopo pembezoni mwa Mto Lumemo lilipojengwa tuta kwaajili ya kuzuia mafuriko.
Aidha Tuta hilo limejengwa kuanzia Kata ya Mbasa hadi Kata ya Lipangalala kutokana na mafuriko yaliyotokea mwaka huu 5/5/2024 .
Katika kuendelea kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi , Shirika la SOLIDARMED limetengeneza bustani kwaajili ya Kupanda miti ya aina mbalimbali katika utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchi .
" Niwapongeze SOLIDARMED kwa hatua hii na nikaribishe wadau mbalimbali waige mfano mzuri wa hawa wadau , waje wachukue eneo kwaajili ya bustani, kila taasisi tuwe na bustani" . Alisema Mhe. Kyobya na kuongeza
" Kwa kufanya hivyo tunalinda Mto Lumemo na kuzuia kutokea kwa mafuriko.
Wakati huohuo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bw. Said Majaliwa alilipongeza Shirika hilo kwa hatua hiyo na kusisitiza Wananchi kuendelea kupanda miti katika maeneo yao.
" Athari za mabadiliko ya Tabia ya Nchi kama tunavyojua huwa ni kubwa , hivyo kila mwananchi ashiriki katika suala Zima la utunzaji wa mazingira ". Alisisitiza Bw. Majaliwa
Kwa upande wake , Mkurugenzi wa Shirika la SOLIDARMED Dkt. Bernatus Sambili alisema Shirika hilo mbali na kufanya shughuli za Afya pia waliamua kushiriki kupanda bustani Ili kulinda Mazingira.
" Tutashiriki shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa miongoni ni hii ambapo tutapanda miti zaidi ya 2000 katika eneo hili". Alieleza Dkt. Bernatus.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa