Maadhimisho ya Wiki ya Elimu yamefanyika Mei 24,2024 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Mang'ula ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe.Dunstan Kyobya.
Aidha maadhimisho hayo yameshereheshwa na Matukio mbalimbali ya Burudani na Michezo.
Hata hivyo taarifa ya kupanda kwa Taaluma imesomwa wakati wa Risala ambapo Taarifa hiyo imeonesha namna gani Taaluma inaimarika kutoka Mwaka 2021 mpaka 2023.
Hali ya Taaluma katika Halmashauri ya Mji Ifakara imeendelea kuimarika kutoka 91.6% 2022 hadi 93.1% 2023 kwa Shule za Msingi na kutoka 88% -2022 hadi 90% -2023 kwa Shule za Sekondari, kwa kuliona Hilo uongozi wa Halmashauri ya Mji Ifakara umewatunukia vyeti vya Pongezi Walimu Mahiri waliofanikisha kupanda kwa Taaluma.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Zahara Michuzi, amewaahidi Walimu kupata stahiki zao za Mapunjo ya Mishahara,Malipo ya likizo na mengineyo ambapo kwa kuanzia Hadi sasa Milioni 90 zimechakatwa ili kulipa baadhi ya Madeni yao.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa