Kutokana na Mlipuko wa Ugonjwa wa Kipindupindu Nchini, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe.Dunstan Kyobya ameongoza zoezi la Usafi maalum katika Soko Kuu la Ifakara Leo Januari 20,2024.
Akizungumza na Wananchi baada ya usafi, DC Kyobya amewataka Wananchi kutumia muda wao kufanya Usafi katika maeneo yao ya makazi na biashara ili kuepuka madhara ya Kipindupindu kitakapojitokeza.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi.Zahara Michuzi akiambatana na Wataalam toka Halmashauri hiyo wameratibu na kushiriki kikamilifu ili kuunga Mkono juhudi za DC Kyobya.
Viongozi mbalimbali wa ngazi zote pamoja na wanajamii kiujumla, wamejitokeza na kujumuika na Wananchi pamoja na Wafanyabiashara wa Soko Hilo wakitumia muda usiopungua masaa matano .
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa