SHIRIKA LA FARM AFRICA KUPITIA MRADI WA KILIMO MASOKO(FARM TO MARKET ALLIANCE)LIMETOA MAFUNZO KWA MAAFISA UGANI NA WAKULIMA VIONGOZI JUU YA KANUNI BORA ZA KILIMO KWENYE ZAO LA MPUNGA.
Mafunzo hayo yalilenga kuwaelimisha Maafisa Ugani pamoja na Wakulima Viongozi wa Halmashauri ya Mji Ifakara kuhusu Mbegu bora kwa kutumia mbegu zilizo na ubora wa hali ya juu kuwa na mgawo bora wa ukuaji na uzalishaji mkubwa.
Pia Afya ya udongo kwa kujifunza umuhimu wa ukaguzi wa udongo, kuongeza rutuba kwa kutumia mbolea zinazofaa, na kudumisha miundo ya udongo ili uzalishaji usiathiriwe vibaya.
Aidha walipata nafasi ya kujifunza usimamizi wa maji kwenye zao la mpunga unahitaji maji kwa wingi, hivyo mafunzo yamekuwa juu ya njia za kusimamia maji vizuri shambani,usimamizi wa umwagiliaji ikiwa ni moja ya mbinu muhimu sambamba na hilo walijifunza Madirisha ya muda wa kilimo Kwa kupanga wakati sahihi wa kupanda, mvua, na kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa ili kuepuka kusabisha upotevu wa mazao pamoja na Udhibiti wa wadudu na magonjwa,uhifadhi baada ya kuvuna.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa