Shule ya Sekondari Msolwa Station yenye namba za usajili *S6252* inayopatikana Kijiji cha Msolwa Station, Kata ya Msolwa Station, Tarafa ya Kidatu katika Halmashauri ya Mji Ifakara.
Shule hii imeanza rasmi mwaka huu 2023 ambapo ujenzi wake ulianzishwa Mwaka 2022 kwa nguvu za Wananchi kwa kuanzisha jengo lenye Madarasa mawili na kupelekea Uongozi wa Halmashauri ya Mji Ifakara kuona haja ya kuunga mkono juhudi za Wananchi kwa kutoa fedha kiasi cha Shilingi Milioni 25 ili kumalizia hatua zilizoanzishwa katika ujenzi.
Kwa utashi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan,Shule hii ilipokea fedha kiasi cha shilingi Milioni 60 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa matatu na kufanya shule iwe na jumla ya Madarasa Matano
Shukrani za dhati zimuendee Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Ndg.Lena Nkaya kwa kufanikisha ukamilishaji wa ujenzi wa Shule hii.
Mpaka sasa wanafunzi wapatao 120 wameondokana na adha ya kutembea umbali mrefu takriban km 10 kwenda Shule ya Sekondari Nyange na km 10 kurudi katika makazi yao ili kuisaka haki yao ya Msingi ya kupata Elimu.
Ni matumaini yetu kuwa Wananchi wataendelea kujitolea katika kutatua changamoto na kuleta Maendeleo yenye tija katika jamii husika na Serikali iko tayari kuwatumikia Wananchi wake kwa kuunga mkono juhudi zao.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa