Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Ifakara limeridhia na kupitisha Rasimu ya mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 kupitia kikao maalum cha Baraza la Bajet kilichofanyika Februari 13,2024 yenye Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Shilingi Bilioni 50.86(Tsh.50,867,773,610.00).
Kati ya fedha hizo Tsh.10,016,886,100.00 ni kwaajili ya Ruzuku ya Miradi ya Maendeleo, Tsh.32,910,590,000.00 ni Mishahara na Tsh.1,352,863,000.00 ni Ruzuku ya Matumizi ya kawaida.
Aidha Tsh.6,587,394,510/= zinatarajiwa kukusanywa toka katika vyanzo vya Mapato ya ndani na kati ya Fedha hizo Tsh.1,969,106,760/= zinatarajiwa kutumika kutekeleza Miradi ya Maendeleo, Tsh.2,953,660,140/= ni za matumizi ya kawaida na Tsh.1,664,627,610/= ni Mapato fungwa.
Jumla ya vipaumbele vimebainishwa katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 ambavyo ni Elimu, Afya,Kilimo Mifugo na uvuvi,Utawala bora,Michezo, Miradi ya kimkakati,TEHAMA na Mawasiliano.
Bajeti hii ya Mwaka wa Fedha 2024/2025 imepanda kutoka Shilingi Bilioni 39.3 ya Mwaka 2023/2024 hadi kufikia Shilingi Bilioni 50.8 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 15
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa