Balozi wa Norway Nchini Tanzania Mhe.Tone Tinnes ametembelea Hifadhi ya Milima Udzungwa Machi 14 2024.
Akiongozwa na Mwenyeji wake ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe.Dunstan Kyobya, Balozi huyo ameweza kujionea uzuri wa Hifadhi hiyo iliyosheheni vivutio vya Utalii kama; maporomoko ya Maji,wanyama na wadudu wa kuvutia.
Hata hivyo Bi.Tinnes amepongeza Mamlaka ya uhifadhi wa Mazingira Nchini kwa kuendelea kutunza Maliasili kwa manufaa ya kizazi kijacho.
"Nmependezwa sana na hali ya uhifadhi ilivyo kwani Mazingira si kwa kizazi hiki tu Bali pia kwa vizazi vijavyo".Alisema Tinnes
Mhe.Tinnes amepata wasaa wakupanda Miti katika Hotel ya Twiga ikiwa ni namna ya kuunga Mkono jitihada za uhifadhi wa Mazingira.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa