Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara Mhe.Kassim F Nakapala amepongeza utekelezaji wa Ujenzi wa Miradi ya Elimu katika ziara ya kamati ya fedha iliyofanyika Januari 22,2024.
Miradi ya Elimu iliyotembelewa ni ujenzi wa; shule ya Sekondari Lipangalala, Matundu ya vyoo shule ya Msingi Ifakara,shule ya Msingi Mlabani na shule ya sekondari Mwanihana, Ofisi ya Walimu shule ya Sekondari Mabukula pamoja na Madarasa shule ya Msingi sanje.
Hata hivyo Nakapala amekemea tabia hatarishi ya ukamilishaji Miradi ya Maendeleo ambayo ni Makadiri ya chini ya gharama za ujenzi inayopelekea uwepo wa madeni .
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi.Zahara Michuzi amemtaka Mhandisi wa Halmashauri hiyo Eng.Michael Ndaga kusimamia kwa karibu Miradi yote ili imalizike kwa wakati na kwa ufanisi.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa