Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya amepokea miche 16,090 ya Kakao, Michikichi , korosho na Karafuu kutoka Shirika la Six Rivers Africa linalojihusisha na uhifadhi wa wanyama pori na kukuza uchumi wa jamii zinazopakana na hifadhi ya Taifa ya Nyerere Halmashauri ya Mji Ifakara.
Miche hiyo imepokelewa leo tarehe 21 Novemba 2024 katika Ofisi za Six Rivers Africa ambapo Mkuu wa Wilaya alilipongeza Shirika hilo kwa uhifadhi wa mazingira na kusema kuwa Miche hiyo itabadilisha maisha ya mtu mmoja mmoja au kikundi na kuwataka Maafisa Maendeleo ya jamii na Wadau wote wa mazingira kuhamasisha na kutoa Elimu ya kutosha kwa Wananchi juu ya uhifadhi wa mazingira.
" Miche hii 16090 inatupa mwongozo wa kipi tufanye badala ya kukata miti haya Mazao ya kakao, korosho, Michikichi na karafuu yatasaidia kuwapa kipato cha mtu mmoja mmoja na mwisho wa siku uhifadhi wa mazingira utafanyika katika maeneo yetu". Alieleza Mhe. Kyobya
Kwa upande wake Bi. Irene Masonda ambaye ni Afisa Mradi wa Shirika la Six Rivers Africa alisema Miche hiyo ni Miche ya kibiashara ambaayo mkulima akichanganya katika shamba lake atakua na uwezo wa kuvuna Mazao mengine kwa muda mfupi.
Aidha , Vijiji vitakavyonufaika na mradi huo ni 12 vilivyopo ndani ya Kata 8 ambavyo ni Katindiuka, Mbasa, Lugongole, sagamaganga, signali, nyamwezi,Mkasu ,bwawani ,mhelule,mikoleko, msalise na miwangani.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa