Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeandaa mkutano maalum na wafanyabiashara Wilayani Kilombero ili kujadili masuala muhimu yanayohusu kodi na biashara.
Mkutano huo uliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero kwa lengo la kuboresha uelewa wa wafanyabiashara kuhusu sheria za kodi, taratibu za ulipaji kodi, na umuhimu wa kufuata sheria hizo kwa maendeleo ya taifa.
"Tunataka Ifakara inayokua yenye hoteli za nyota tano,kumbi nzuri za mikutano na tuone ni Kwa namna gani tunaenda kuboresha hadhi ya Halmashauri ya Mji Ifakara na Wilaya ya Kilombero kwa ujumla."Mhe.Wakili Dunstan Kyobya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero
Katika mkutano huo, wafanyabiashara walipata fursa ya kuuliza maswali na kutoa maoni yao kuhusu changamoto wanazokutana nazo katika biashara zao hasa suala la ulipaji wa kodi.
Meneja wa TRA Wilaya ya Kilombero Bw. Wilfred Makamba alitoa elimu na ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya kikodi, ikiwa ni pamoja na:
Jinsi ya kujisajili na kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN),Taratibu za kuandaa na kuwasilisha ritani za kodi sambamba na hilo Mbinu za kuepuka adhabu na riba kutokana na ucheleweshaji wa malipo ya kodi Vilevile alieleza Faida za kutumia mfumo wa kielektroniki katika ulipaji wa kodi.
"Sisi kama Mamlaka ya mapato ni jukumu letu kuwahudumia wananchi na kusimamia vile Sheria inataka na kama mnapata huduma ambayo inakinzana na sheria basi msisite kutoa taarifa ili tuweze kutatua changamoto zenu pia Kila mmoja ajue Haki zake katika ulipaji wa kodi "alisema Makamba
Aidha TRA inawahimiza wafanyabiashara wote Wilayani Kilombero kuhudhuria mikutano mbalimbali ili kupata taarifa sahihi na za kina kuhusu masuala ya kodi,Ushiriki wao utasaidia kuboresha uhusiano kati ya TRA na wafanyabiashara, na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa