Na: Nuru Mangalili – Ifakara Tc , Habari
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Pilly Kitwana amewataka Maafisa Elimu Kata na Wakuu wa Shule za Sekondari kuhakikisha wanasimamia vizuri Miradi ya Maendeleo katika Shule zao.
Hayo ameyasema tarehe 9 Julai 2025 wakati alipofanya Kikao na Maafisa Elimu Kata na Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali na Binafsi zilizopo Halmashauri ya Mji Ifakara.
“Kila mmoja atekeleze wajibu wake, kama umeletewa miradi kwenye eneo lako hakikisha kwa kufuata taratibu na miongozo miradi ikamilike kwa wakati . Huu ni mwaka mpya wa Fedha, kuna fedha zitaletwa kwaajili ya Miradi muhakikishe mnakua wasimamizi wazuri wa Miradi hiyo”. Alisema Bi. Pilly Kitwana
Aidha Bi. Pilly Kitwana aliwasisitiza Waratibu hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa kufuata taratibu , miongozo, sheria na maadili ya Utumishi wa Umma , kuhakikisha wanaongeza ufaulu wa wanafunzi na Mahusiano mazuri kazini.
Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bw. Folkward Mchami alisisitiza Waratibu hao wa Elimu kuhakikisha hakuna Mwanafunzi atakaye pata Divisheni Ziro katika Halmashauri ya Mji Ifakara.
“ Tunampango wa kufuta Divisheni Ziro, katika kila Shule, hivyo Walimu tuhakikishe wanafunzi wote wanafaulu kwa kuondoa utoro mashuleni na kuhakikisha walimu wanafundisha vipindi vyote kwa weledi”. Alieleza Bw. Mchami
Bi. Pilly Kitwana alisiskiliza changamoto na kero mbalimbali za Waratibu hao wa Elimu na kuzipatia ufumbuzi
.
Wakati huohuo Bw. Bonaventure Nyoni Afisa Elimu Kata ya Mkula alimshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Pilly Kitwana kwa Kikao hicho na kuahidi kuondoa Ziro Mashuleni Pamoja na kusimamia vizuri miradi.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa