Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt . Damas Ndumbaro ( Mb) amesema Migogoro yote iliyopo katika Wilaya ya Kilombero inapaswa kuisha kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia( Mama Samia Legal Aid Campaign) kwa kuwa kila mwananchi mwenye Mahitaji anatakiwa apate Msaada wa Kisheria .
Hayo ameyasema mapema leo Disemba, 14, 2024 wakati akifungua Kampeni ya Mama Samia ya Msaada wa Kisheria katika Wilaya ya Kilombero ambapo alisema Msaada huu wa Kisheria ni maelekezo Mahususi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye aliona kero na changamoto zinazowakuta watanzania katika masuala ya Sheria na utatuaji wa Migogoro,hivyo akaagiza Wizara yenye dhamana inayohusika na Katiba na Sheria ,iandae mpango wa Msaada wa Kisheria Bure kwa watanzania wote.
"Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza kila mwananchi mwenye Mahitaji apate Elimu na msaada wa kisheria ,Wataalamu wapo kwa muda wa siku 9 Wilayani Kilombero na watahakikisha kila mwananchi mwenye kero anasikilizwa na kutatuliwa kero yake". Alieleza Mhe. Dkt. Ndumbaro
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya alimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kuleta Elimu na huduma ya Kisheria ya Mama Samia buree katika Wilaya ya Kilombero kwani Wananchi watatauliwa masuala mbalimbali ikiwemo migogoro ya wakulima na Wafugaji, mirathi , ndoa, unyanyasaji wa kijinsia n.k.
Aidha , Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilombero Ndugu . Mohammed Msuya aliwataka Wananchi wa Kilombero Kujitokeza kwa wingi katika siku 9 za Wataalamu hao wa Sheria watakazo kuwepo Wilayani Kilombero.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa