Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Mohamed Mchengerwa amefanya Ziara ya katika Mji wa Ifakara Mei 20,2024.
Katika Ziara hiyo Mhe.Mchengerwa amekagua Jengo la Hospitali ya Halmashauri ya Mji Ifakara Kiberege na kuongea na Wananchi wa Kata ya Kiberege.
Aidha Mhe.Mchengerwa amewataka Viongozi wa Halmashauri hiyo kusimamia Mradi huo na kuhakikisha unakamilika kabla ya Agosti 1,2024.
Hata hivyo ameahidi kufika katika Kata hiyo wakati wa uzinduzi wa Jengo hilo pamoja na kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Daraja la Mkasu ambalo ni kilio kikubwa kwa Wananchi.
Katika hatua Nyingine Mhe.Mchengerwa ameitaka TARURA kukarabati Barabara za Kata hiyo ili kurahisisha shuhuli za usafiri na usafirishaji kwa Wananchi kama Diwani wa Kata ya Kiberege Mhe.Sultan Kwanja alivyoomba kwa niaba ya Wananchi wake.
Si hayo tu lakini pia Mhe. Mchengerwa amewaahidi Wananchi wa Ifakara kuhakikisha wanapata Shule ya Ghorofa mbadala wa Shule ya Msingi Kibaoni ambapo kwasasa inamrundikano wa Wanafunzi na haina eneo la kutosha la Kuongeza zaidi Majengo ya Madarasa.
Ahadi hiyo imetokana na Ombi la Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mhe.Abubakar Asenga pamoja na Diwani wa Kata ya Ifakara Mhe.James Uliza katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Soko Kuu la Ifakara uliokamilisha Ziara.
Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mhe.Abubakar Asenga
Diwani wa Kata ya Ifakara,Mhe.James Uliza
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa