Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara, Bi. Witness Kimoleta, amefunga mafunzo ya mfumo wa GOTHOMIS CENTRALIZED.
Mafunzo hayo yalifanyika kwa siku kumi ambapo wataalamu wa Afya kutoka tarafa ya Mang'ula walipatiwa mafunzo, na hatimaye yakahitimishwa katika tarafa ya Kidatu katika Kituo cha Afya Mkamba.
Msimamizi wa mafunzo hayo Bw. John Mvanga, alisema kuwa kupitia mafunzo hayo, wataalamu wote walioshiriki wamepatiwa uelewa wa kutosha na wanakwenda kuongeza makusanyo na tija katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha, Bi. Kimoleta amewapongeza wataalamu wote wa TEHAMA na Afya kwa kazi nzuri waliofanya katika kuongeza mapato ya idara ya Afya. Alisisitiza umuhimu wa kuongeza uwezo wa kufanya kazi kisayansi na kuhakikisha kuwepo kwa data sahihi.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa