Katika kuhakikisha shughuli ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura inafanyika kwa ufanisi, mafunzo maalum yameandaliwa kwa watendaji wa ngazi ya jimbo kufuata taratibu, sheria, na miongozo inayohusiana na uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Aidha katika Mafunzo hayo Watendaji walijifunza
zinazoweza kujitokeza wakati wa z kuwajengea Uelewa wa miongozo ya kisheria kuhusu usajili wa wapiga kura,Mbinu za uhakiki wa taarifa kupitia njia bora za kuthibitisha na kusahihisha taarifa za wapiga kura vilevile Matumizi sahihi ya Teknolojia hasa kwa ujuzi wa kutumia vifaa vya kisasa katika kuboresha daftari la wapiga kura.
Mafunzo haya yanawapa maarifa ya kutumia teknolojia mpya inayotumika katika kuhakiki, kusajili, na kurekebisha taarifa za wapiga kura,hata hivyo Ushirikishwaji wa jamii Kwa Kuangalia namna ya kuwahamasisha wananchi kushiriki katika zoezi la uboreshaji wa daftari sambamba na hilo
Udhibiti wa changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa zoezi hili
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi.Pilly Kitwana aliwataka watendaji hao kufanya kazi kwa kufuata kanuni, taratibu na Sheria za uchaguzi katika kuboresha daftari la wapiga kura.
"Hili ni zoezi kubwa kitaifa na nyie mmeaminiwa na kuteuliwa Kwa ajili ya shughuli hii basi niwaombe mwende mkasikilize vizuri mafunzo haya ili muweze kutekeleza adhma na makusudio ya Tume ya Taifa ya uchaguzi,"amesema Bi.Pilly Kitwana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa