Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki (BVR) Jimbo la Kilombero Februari 26 ,2025 wamepatiwa Mafunzo kuelekea zoezi hilo linalotarajiwa kufanyika kuanzia 1-7 Machi 2025 katika Vituo mbalimbali ndani ya Kata zote 19 za Jimbo la Kilombero.
Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha wahusika kupata ujuzi wa kina kuhusu matumizi sahihi ya vifaa vya BVR, usimamizi wa taarifa za wapiga kura, na kuhakikisha usahihi wa taarifa ili kuepusha dosari zinazoweza kuathiri mchakato wa uchaguzi. Vilevile kuhimiza uadilifu, uwajibikaji, na weledi katika kutekeleza majukumu yao.
Aidha, Mratibu wa Uandikishaji wa Mkoa wa Morogoro Bw. Herman Tesha aliwasisitiza Washiriki hao kuwa wasikivu na Makini katika Mafunzo hayo Ili wakafanye Kazi kwa weledi katika Vituo watakavyokwenda kufanyia Kazi na kuhakikisha kila mmoja anatunza vizuri vifaa hivyo vya zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura
.
" Hili ni suala muhimu kitaifa muhakikishe mnaongeza umakini na Uadilifu wa hali ya Juu, mkazingatie Sheria , kanuni na weledi katika zoezi hili. " Alieleza Bw. Tesha.
Mgeni Rasmi katika Mafunzo hayo alikua Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Pilly Kitwana ambaye aliwataka Wasaidizi hao kuhakikisha wanafuta yale watakayofundishwa katika semina hiyo Ili zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga kura lifanyike kwa weledi.
Jumla ya Washiriki 634 wamepatiwa Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza leo tarehe 26 Februari 2025 na kuhitimishwa hapo kesho tarehe 27 Februari 2025.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa