Watendaji wa Kata,Vijiji na Mitaa wa Halmashauri ya Mji Ifakara, Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba pamoja na Ulanga wamepatiwa mafunzo ya maadili na utaratibu wa kazi za utumishi wa umma.
Mafunzo hayo walipatiwa na wawezeshaji kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo cha Jijini Dodoma,leo Januari 6/2025 katika Halmashauri ya Mji Ifakara.
Afisa Utumishi Mwandamizi kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Bw. Beyond Samwel Madege aliwataka watendaji hao kuheshimu sheria,utaratibu pamoja na kutunza Siri za Ofisi ikiwemo kufuata maadili ya Utumishi wa Umma.
"Watendaji mnatakiwa kufuata taratibu za Utumishi wa Umma na kuwa waadilifu kazini pia mkaepuke vitendo vyenye kuchafua sifa ya Utumishi,"alisema Madege.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe.Wakili Dunstan Kyobya amewataka watendaji hao kujenga Mahusiano mazuri baina yao na wananchi ili kuweza kutoa huduma bora na kuleta maendeleo katika jamii Kwa pamoja.
Dc Kyobya aliongeza kuwa anahitaji Watendaji hao kwenda kusimamia mapato na Miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kata na Mitaa yao pia wakahakikishe wale wote wanaofanya kazi zao ndani ya mita 60 usawa wa vyanzo vya maji kuacha kufanya shughuli zote za kijamii katika eneo hilo.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa