Viongozi wa Soko Kuu la Ifakara, wameridhia eneo lililotengwa na Halmashauri ya Mji Ifakara, kupisha ujenzi wa Soko la Kisasa ifikapo Machi 2024.
Maridhiano hayo yamefanyika Tarehe 29 Disemba 2023 kati yao na Wataalamu wa Halmashauri ya Mji Ifakara baada ya kutembelea katika eneo ambalo litajengwa soko hilo wakiwa wameambatana na viongozi wa Mtaa.
"Tumeridhishwa na ukubwa wa eneo la Uwanja wa Kiungani ili kupisha ujenzi wa Soko utakapoanza japo ombi letu ni kuboreshewa Miundombinu inayokidhi mahitaji ya Wafanyabiashara". Joseph Haule, Mwenyekiti wa Soko kuu la Ifakara.
Soko la Ifakara linatarajiwa kujengwa kisasa kwa zaidi ya Shilingi Bilioni 3 kwa muda wa Mwaka mmoja, kupitia Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Miji Tanzania - TACTIC.
Hii ni baada ya maridhiano ya Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Ifakara na Wataalamu wa Halmashauri ya Mji Ifakara yaliyofanyika Tarehe 7 Septemba 2023.
Matukio katika Picha:
Timu ya Wataalamu kutoka Halmashauri ya Mji Ifakara, Viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Kiungani na Viongozi wa Soko Kuu la Ifakara wakiwa katia eneo ambalo Wafanyabiashara wa Soko hilo watahamishiwa kwa muda ili kupisha ujenzi wa Soko jipya la Ifakara.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa