Maafisa Afya wa Halmashauri ya Mji Ifakara wametoa Elimu kwa Mama lishe na Baba lishe katika kata ya Ifakara na Kibaoni Januari 17,2024
Katika ukaguzi huo Mama/Baba lishe wametakiwa ;Kuwa wasafi binafsi na Mazingira,Kufunikia vyakula na kuwapa wateja wao vyakula vya moto pamoja naKuwa na Ndoo ya Maji moto tiririka na Sabuni kwa ajili kunawa mikono kabla na baada ya kula.
Sambamba na hayo Maafisa hao wameendelea kutoa Elimu hiyo kwa Wanafunzi wa Shule mbalimbali za Msingi na Sekondari .
Zoezi hili ni endelevu likilenga kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Kipindupindu kwa kuwapa Elimu ya Afya Makundi mbalimbali katika jamii.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa