Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe.Wakili Dunstan Kyobya leo februari 3,2025 amezitaka taasisi zote zinazosimamia kesi za madai kutenda haki pia wafanye kazi Kwa weledi,uadilifu pamoja na uwajibikaji kama Kauli mbiu ya Mahakama inavyosema.
DC Kyobya ameyasema hayo katika Kilele cha wiki ya Sheria, ambapo aliwataka Mawakili hasa wa kujitegemea kuwa na utaratibu wa kutoa msaada wa kisheria bure Kwa wananchi ili kuweza kutatua changamoto zao hata hivyo amewapongeza Mawakili Kwa kazi nzuri wanayofanya Halmashauri ya Mji Ifakara na Wilaya ya Kilombero kwa ujumla.
Aidha Mhe.Wakili Kyobya amewataka Mawakili wasio na vigezo maarufu kama (Vishoka) kuacha kujihusisha na utoaji wa huduma za kisheria na endapo watabainika kuendelea na kazi hiyo hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao pia ameongeza kuwa wananchi wanatakiwa kuelimshwa ili kusimamia haki zao.
" Niwaombe OCD,Mhe.Hakimu Mfawidhi Pale ambapo mtaona mtu anafanya shughuli za kisheria na hana leseni maarufu (Vishoka) basi mchukue hatua na mhakikishe haki inatendeka,"amesema DC Kyobya.
Hata hivyo Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Kilombero Mhe.Regina Futakamba amesema kuwa wiki ya Sheria ni fursa Muhimu Kwa wananchi kupata elimu ya masuala mbalimbali ya sheria pamoja na kupata msaada wa kisheria bure ikiwemo Usimamizi wa Mirathi,uandishi wa Wosia, Haki Jinai nk.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa