Mkuu wa wilaya ya kilombero Wakili Dunstan kyobya, Amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya(OCD) Kuhakikisha Anachukua Hatu Kali Dhidi ya Wale Wote Aliowaita Mawakili Vishoka Kwa Kuchafua na Kuharibu Dhana ya Uwakili na Taaluma ya Sheria Kwa Ujumla Katika Jamii na Badala Yake.
Ameyasema hayo Februari 1,2024 katika Maadhimisho ya wiki ya Sheria yaliyoadhimishwa viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Kilombero.
DC Kyobya Ametaka Uwepo wa Mawakili Wenye Sifa Stahiki na Weledi Watakaoweza Kuwasaidia Wananchi Katika Kutafuta Haki zao.
Hata hivyo Chama cha Mawakili Tanganyika Wilaya ya Kilombero wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan Kwa kuboresha Mifumo ya haki jinai kwa ustawi wa Taifa.
Maadhimisho hayo yameongozwa na kauli mbiu inayosema
"Umuhimu wa Dhana ya haki kwa ustawi wa Taifa:Nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha Mfumo jumuishi wa Haki jinai"
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa