Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe.Dunstan Kyobya ameendesha kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Halmashauri ya Mji Ifakara leo Februari 10,2024.
Kikao hicho chenye lengo la kutangaza kampeni ya Chanjo ya Surua Rubella kimehudhuriwa ma Viongozi mbalimbali wa chama na Serikali.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kilombero
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara Mhe.Kassim F Nakapala
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Adv.Florida Kimambo
Hata hivyo DC Kyobya ametoa wito kwa wajumbe wa Kamati hiyo kucheza vizuri katika nafasi zao ili jamii iwe na uelewa mpana juu ya chanjo hiyo.
Naye Mratibu wa Chanjo wa Halmashauri ya Mji Ifakara Stephen Simbeye ametanabaisha kuwa Chanjo hii itatolewa tarehe 15 - 18 Februari 2024 kwa watoto wenye umri chini ya Miaka Mitano.
Si hayo tu lakini pia Chanjo itatolewa kupitia Vituo vyote vya Afya vinavyotoa huduma za mama na mtoto pamoja na Mashuleni.
Hivyo wazazi wameaswa kutoa ushirikiano wa kutosha kwani Surua na Rubella haina Tiba.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa