Kikao cha Afya ya Msingi ( PHC) kwaajili ya kujadili Hali ya Ugonjwa wa Homa ya Tumbo kimefanyika leo Tarehe 18 Disemba Katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Halmashauri ya Mji Ifakara.
Aidha , katika Kikao hicho mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwemo mpango mkakati wa kuzuia na kudhibiti Ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa Elimu kwa jamii kupitia vikao mbalimbali vya ngazi ya Kata, Vijiji na Vitongoji na Pia kuhamasisha njia mbalimbali za usafi kwa Wananchi Ili kuendelea kujikinga na kuepukana na Ugonjwa huo.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi wa Dini, Mashirika, Viongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji, Maafisa Ustawi wa Jamii, Maafisa Afya , Viongozi wa Tiba Asili na Tiba Mbadala n.k
Mwenyekiti wa Kikao hicho alikua Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya.
Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bibi. Witness Kimoleta aliwataka Wadau na Viongozi hao kushurikiana Ili kufanikisha mikakati iliyowekwa ya kujikinga na kuondokana na Ugonjwa huo.
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa