Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe.Dunstan Kyobya amewataka maafisa ugani, Kilimo ,mifugo, Uvuvi na Maendeleo ya Jamii kusimamia majukumu yao ipasavyo katika Jamii ili kuleta Maendeleo katika Halmashauri ya Mji Ifakara na Wilaya ya Kilombero kwa ujumla.
Hayo ameyasema leo Septemba 6, 2024 katika Kikao Kazi alichokua akifanya na Maafisa Ugani, Kilimo, Mifugo , Uvuvi na Maafisa Maendeleo ya Jamii katika Ukumbi wa Mlimba uliopo Halmashauri ya Mji Ifakara.
" Maafisa Kilimo kasimamieni bei za Mazao, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha Kilimo cha mbogamboga na matunda kwa wananchi na vilevile mkahamasishe Wananchi waandae vitalu vya miti inayotunza mazingira kama vile miti ya michikichi ,mikokoa , mikarafuu , mikorosho nk" . Alisema Mhe. Kyobya
"Wote tukisimamia majukumu yetu vizuri, Wilaya yetu itapata Maendeleo makubwa". Alisisitiza Mhe. Kyobya
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa