Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara Mhe.Kassim Nakapala, ameiongoza Kamati ya fedha na utawala katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
Kamati hiyo imepata wasaa wa kutembelea baadhi ya Miradi ya Afya inayoendelea kutekelezwa kama Zahanati ya kijiji cha Mpanga kilichopo kata ya Kisawasawa kinachotarajiwa kuhudumia wananchi zaidi ya 1500 mara baada ya kukamilika ambao kwa sasa wanapata huduma hiyo katika kituo cha Afya Mang'ula kilichopo umbali wa km 38 kutoka katika maeneo yao ya makazi.
Hata hivyo wajumbe wa Kamati ya fedha wameweza kukagua Miradi ya Elimu kama; ukarabati wa Madarasa mawili katika Shule ya Msingi Ichonde na ujenzi wa madarasa mawili na ofisi ya Walimu katika Shule ya Msingi Sanje.
Ziara ya kamati ya Fedha imefanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 18/10/2023 mpaka tarehe 19/10/2023
Kibaoni - Bomani
Sanduku la Barua: 433 Ifakara
Simu ya Mezani: +255 (0)23 - 2934212
Simu ya Mkononi: -
Barua Pepe: td@ifakaratc.go.tz / info@ifakaratc.go.tz
Haki Miliki @2018 Halmashauri ya Mji wa Ifakara . Haki zote zimehifadhiwa